Tuma barua pepe kwenda gettor@torproject.org.
Katika ujumbe wa barua pepe, andika jina la mfumo wa uendeshaji (kama vile Windows, macOS, au Linux).
GetTor itajibu kwa barua pepe iliyo na anwani unayoweza kupakua Tor Browser, sahihi ya picha (itahitajika kuthibitisha upakuaji), fingerprint ya funguo iliyotumika kuwekea sahihi, na kifurushi cha checksum.
Unaweza kupewa chaguo la programu ya "32-bit" au "64-bit": hii itategemea na aina ya kompyuta unayotumia, angalia nyaraka kuhusu kompyuta yako ili kujua zaidi.